Lengo letu kubwa lilikuwa kwamba tuweze kuwafikishia watu hadith za Bukhari kwa Kiswahili ili wale wanaojua lugha ya Kiswahili waweze kunufaika nazo.
Bado kuna watu wengi wanahitaji kufikishiwa hadith hizi; kuna vipofu, viziwi na kadhalika. Siyo ujanja wetu kwamba tunaweza tukaona na siyo ujanja wetu kwamba tunaweza tukasikia.
(Update yamliku na elezea maana ya riziki kwa kiarabu kwenye 10:31)
Sema: Ni nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Au ni nani anaye miliki kusikia na kuona? Na nani amtoaye hai kutoka maiti, na akamtoa maiti kutoka aliye hai? Na nani anaye yadabiri/panga/kadiria mambo yote? Watasema: Allah. Basi sema: Je! Hamchi? (Qur’an 10:31)
Kama tulivyokuwa hatuwezi kusikia jinsi watu wanavyoadhibiwa kaburini, kuna wengine hawawezi kusikia sauti (yoyote) [yani viziwi]; lakini hao wanaweza kusaidiwa kwa kufikishiwa ujumbe kupitia uwezo wao wa kuona. Mfano mtu anaweza akarekodi kila hadith ya Bukhari a nambari yake ili kiziwi aweze kuangalia/kusoma.
Kama tulivyokuwa hatuwezi kuona Malaika, kuna wengine hawawez kuona kitu (chochote) [yani vipofu]; lakini hao wanaweza kusaidiwa kwa kufikishiwa ujumbe kupitia uwezo wao wa kusikia. Mfano mtu anaweza akarekodi kila hadith ya Bukhari na nambari yake ili kipofu aweze kuzisikiliza/kusoma. Kama anaelewa Kiarabu atasikiliza audio ya Kiarabu kwa kuwa hapo ndo uhalisia wake upo, kwa lugha zingine inakuwa maana inapotea kwa asilimia fulani. Kama anaweza akashika shika vile vitabu vyenye herufi zao na akaelewa, basi hiyo nayo ni nzuri.